Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Chuo Kikuu kione aibu wahitimu wakichoma mahindi barabarani: Rais Ruto

Chuo Kikuu kione aibu wahitimu wakichoma mahindi barabarani: Rais Ruto

0 comment 226 views

Rais wa Kenya William Ruto amevitaka vyuo nchini humo kuzalisha wahitumu wanaoajirika.

Amesema wanaangalia namna ya kuboresha kozi na aina ya ufundishaji katika vyuo na ubora wa wahitimu wanaozalishwa na vyuo husika.

Rais Ruto amevitaka vyuo nchini humu kuboresha ufundishaji na kusema kama wanatumia pesa za umma, umma unatakiwa upate thamani kwa kila Shilingi ya serikali inayotumika katika kila chuo na kila mwanafunzi.

“Tunaenda kusisitiza kuwa haitoshi tuu kwa chuo kuzalisha mhitimu, wanatakiwa kujua kama huyu mhitimu amepata mafunzo sahihi na je anaweza kuajiriwa katika soko la ajira,” amesisitiza Rais Ruto.

Amesema kama chuo kinazalisha wahitimu wanaochoma mahindi kandokando ya barabara hakistahili kupata rasilimali za umma.

“Chuo kione aibu kuona wahitimu wake wanachoma mahindi barabarani, na kama hakioni aibu basi hapo kuna tatizo,” amesema Rais Ruto.

“Vyuo vinatakiwa kuwafatilia wahitimu wao, kujua kozi wanazofundisha na uhitaji katika soko la ajira na uchumi wa nchi na mipango ya maendeleo ili tusijekuzalisha wahitimu ambao hawana sehemu sahihi katika uchumi wetu.

Tusije tukachangia kuongeza tatizo la ukosefu wa ajira kwa sababu tumetengeneza wahitimu ambao hawaajiriki kutokana na aina ya kozi walizofundishwa,” amesema Rais Ruto.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter