Home VIWANDANISHATI Tanzania, Msumbiji kushirikiana kwenye gesi na mafuta

Tanzania, Msumbiji kushirikiana kwenye gesi na mafuta

0 comment 87 views

Tanzania na Msumbiji zimeingia makubaliano ya usafirishaji wa mafuta na gesi.

Ushirikiano huo unakuja baada ya Rais wa Tanzania kutembelea nchi ya Msumbiji na kujadili mambo mbalimbali na Rais wa nchi hiyo Felipe Nyusi.

Mkurugenzi wa Biashara, Mafuta na Gesi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Wellington Hadson ameeleza hayo wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano hayo.

Amebainisha kuwa “tutakumbuka Septemba mwaka jana, Rais wetu Samia Suluhu Hassan alifanya ziara ya kwenda Msumbiji, ambapo pamoja na mambo mengine alikuwa na mazungumzo na Rais Felipe Nyusi.”

Amesema ushirikiano huo utarahisisha usafirishaji wa bidhaa hizo na hivyo nchi husika kupata faida zaidi.

Nae Mkurugenzi wa Shirika la Mafuta nchini Msumbiji, Estevao Pale amesema mbali na ushirikiano katika usafirishaji pia watabadilishana wataalamu wa sekta hizo.

Amesema ushirikiano huo pia utahusisha sekta nyingine nyingi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter