Home VIWANDANISHATI Korea Kusini yaunga mkono matumizi nishati safi ya kupikia

Korea Kusini yaunga mkono matumizi nishati safi ya kupikia

0 comment 58 views

Mkakati wa Nishati Safi ya kupikia chini ya uasisi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan umeendelea kupigiwa chapuo ambapo Korea Kusini imesema iko tayari kuunga mkono jitihada hizo.

Hayo yameelezwa Machi 6, 2025 katika mazungumzo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko na Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Ahn Eunju kando ya Mkutano wa Mafuta na Gesi kwa nchi za Afrika Mashariki unaoendelea jijini Dar es Salaam.

Dkt. Doto Biteko amesema Tanzania imepiga hatua katika kuwezesha wananchi kupata unafuu wa maisha kwa kupata na kutumia nishati safi na hivyo kuepukana na madhara yanayotokana na matumizi ya nishati isiyokuwa safi yakiwemo magonjwa na vifo.

Mkakati wa Taifa wa Nishati safi ya kupikia wa miaka 10 unakusudia kuwawezesha asilimia 80 ya Watanzania kuwa watumiaji wa nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

“Tunaendelea kutekeleza mkakati huu kwa kubadilisha mtazamo wa watu waliokuwa wakitumia vyanzo vya asili vya nishati ambavyo sio salama, lakini tunaendelea kubadili mitazamo yao ili waweze kuungana na jitihada hizi za kitaifa na kimataifa za matumizi ya nishati safi ya kupikia.” amesema Dkt. Biteko.

Amesema kuna jitihada mbalimbali kimataifa ikiwemo kusainiwa kwa makubaliano kuhusu matumizi ya nishati kwa lengo la kuwezesha upatikanaji wa nishati safi kwa gharama nafuu.

Aidha, amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya serikali na Sekta binafsi hauepukiki ili kufikia malengo yaliyokusudiwa

“Katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi Barani Afrika tulisaini makubaliano kadhaa ikiwa ni pamoja na kupata fedha ili kuwawezesha wahitaji kuboresha maisha yao kupitia Nishati Safi” amesema Dkt. Biteko.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter