Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI 44.4bn kutumika matumizi ya kawaida na maendeleo

44.4bn kutumika matumizi ya kawaida na maendeleo

0 comment 136 views

Serikali ya Tanzania imepanga kutumia jumla ya Sh. bilioni 44,388.1 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo.

Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 29,232.1 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikijumuisha shilingi bilioni 12,771.5 kwa ajili ya ulipaji wa deni la Serikali na gharama nyingine za Mfuko Mkuu na shilingi bilioni 10,882.1 kwa ajili ya mishahara ikiwemo upandishaji wa madaraja kwa watumishi na ajira mpya, na shilingi bilioni 6,396.9 kwa ajili ya matumizi mengineyo (OC).

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba ameeleza hayo wakati akiwasilisha mbele ya Bunge Jijini Dodoma, Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2023/24.

Mpango huo umeonyesha kuwa matumizi ya maendeleo yanatarajiwa kuwa Sh. bilioni 15,156.0. Kati ya kiasi hicho, Sh. bilioni 11,873.9 ni fedha za ndani, sawa na asilimia 78.3 ya bajeti ya maendeleo na shilingi bilioni 3,282.1 ni fedha za nje.

Ukomo wa fedha za maendeleo upo ndani ya wigo wa kati ya asilimia 30 na 40 ulioanishwa kwenye Mpango Elekezi wa Muda Mrefu (2011/12 – 2025/26).

Utengaji wa fedha za maendeleo umezingatia miradi inayoendelea ikiwemo miradi ya kimkakati na ya kielelezo pamoja na utekelezaji wa miradi kupitia utaratibu wa Publi Private Partnership (PPP) ili kuipunguzia Serikali mzigo wa kugharamia miradi ya maendeleo kwa utaratibu uliozoeleka.

Aidha, bajeti ya matumizi ya kawaida imeongezeka kufuatia kukamilika kwa miradi ya maendeleo hususan kwenye sekta za huduma za jamii ambazo kwa sasa zinahitaji fedha za matumizi ya kawaida kwa ajili ya uendeshaji.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter