Home BIASHARA Ujenzi wa masoko kushirikisha machinga

Ujenzi wa masoko kushirikisha machinga

0 comment 75 views

Ili kuepuka ujenzi wa masoko usio rafiki kwa biashara, Halmashauri nchini zimetakiwa kushirikisha viongozi wa machinga wa eneo husika kabla ya kufanya ujenzi.

Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam ambae pia ni mlezi wa Machinga CPA, Amos Makalla amesema hayo akizungumza na maelfu ya Machinga kwenye Kongamano lililofanyika Ukumbi wa PTA Sabasaba.

“Chukueni mawazo ya viongozi wa machinga ili kuepuka kujenga masoko yasiyo rafiki kwa bishara,” amesema RC Makalla.

Katika kongamano hilo RC Makalla amewahakikishia wafanyabiashara kuwa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kulea na kulinda kundi hilo ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira yao.

Aidha, amewaelekeza wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na maafisa Biashara kuhakikisha kila soko linakuwa na maji na vyoo na kuwataka kufanyika vikao vya mara kwa mara ili kujua changamoto zao.

RC Makalla amewaelekeza Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kuhakikisha wanaweka route za daladala kwenye kila soko ili kuchagiza Biashara.

Akizungumzia hatma ya wafanyabiashara soko la Kariakoo walioondolewa kupisha ujenzi baada ya soko hilo kuungua, RC Makalla amesema soko likikamilika kipaumbele cha kwanza kitakuwa kwa wazawa waliokuwepo na kueleza kuwa mwelekeo baada ya soko kukamilika ni biashara saa 24.

Pamoja na hayo RC Makalla amewaelekeza Wakurugenzi kuhakikisha kipaumbele cha mikopo ya asilimia 10 inatolewa kwa wanaofanya shughuli za machinga.

Hata hivyo RC Makalla ametoa wito kwa taasisi za fedha kuwafikia machinga na kuendelea kutoa mikopo rafiki kwa wafanyabiashara.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter