Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde amewaeleza wadau wa vanila namna Serikali ilivyojipanga kufanya utafuti wa mazao likiwemo zao la vanila.
mavunde amesema hayo wakati akifungua mkutano wa Wadau wa Zao la Vanila nchini.
Amesema Vanila ni moja ya mazao yanayoweza kuwekewa mkakati ili kuongeza uzalishaji na uuzaji kwenye soko la kimataifa.
“Jambo kubwa ni kuhakikisha zao hili la vanilla liwe katika utaratibu mzuri kwa kutengenezewa muongozo ambao utatusaidia kujibu hoja nyingi sana ambazo zimewasilishwa hapa.
Tumefanya hivi katika mazao mengi sana ya mbogamboga na matunda, tumekamilisha mwongozo wa parachichi ambayo nayo ilikuwa changamoto kubwa, hamasa kwa wakulima ilikuwa ni kubwa lakini walikuwa wanakwenda bila kuongozwa na ilitupelekea kupata changamoto nyingi sana pamoja na kupata notification nyingi sana kama nchi ambazo zilikuwa pia zinaathiri soko letu la kimataifa la mazao ya kilimo,” ameeleza.
Asemema hali hiyo ilikuwa inaatarisha soko la Tanzania la mazao ya kilimo
Amesema moja kati ya changamoto kubwa ilikuwa ni mfumo wa mnyororo wa ubaridi wa uhifadhi mazao ya mbogamboga na matunda.
Kuhusu kutambulika kwa ubora wa mazao ya kilimo katika viwango vya kimataifa Mavunde amesema tayari Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viwatilifu (TPHPA) imeshapata ithibati za kimataifa ambayo inathibitisha ubora wa mazao kimataifa.