Home BIASHARA Kushiriki maonesho China Dola 3,000

Kushiriki maonesho China Dola 3,000

0 comment 81 views

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imetangaza fursa kwa wafanyabiashara wa Tanzania wanaotaka kushiriki Maonesho makubwa ya Kimataifa ya biashara nchini China yajulikanayo kama Canton Fair.

Kwa mujibu wa TanTrade gharama za kushiriki ni Dola za Marekani 3,000 kwa kila mshiriki.

Gharama hizo zitahusisha usafiri wa ndege daraja la uchumi, usafiri wa ndani (ground transport), malazi katika hoteli ya nyota 4 kwa siku 7.

Zingine ni matembezi ya viwandani na masokoni, mkutano wa jukwaa la biashara, Visa na kiingilio cha maonesho ambapo wataondoka kwa awamu tatu.

Awamu ya kwanza ya wafanyabiashara itaondoka Dar es Salaam Aprili 13 na kurudi Aprili 20, 2023 ambapo itahusisha wafanyabiashara wa vifaa vya majumbani na ujenzi.

Ya pili itahusisha wafanyabiashara wa bidhaa za chakula (consumer goods, gifts, home decorations) itaondoka Aprili 22 na kurudi Aprili 29, 2023.

Ya tatu Aprili 29 na kurudi Mei 6, 2023 ambayo itahusisha bidhaa za ngozi, viatu, vifaa vya maofisini, madawa, huduma za matibabu, mikoba na mabegi.

“Kwa kushirikiana na ofisi ya Konseli kuu ya Tanzania jijini Guangzhou na Jumuiya ya Watanzania GuangDong (Ditag) wanapenda kuwaalika Watanzania wote wenye kuuza nje ya nchi na kununua bidhaa China, wawekezaji na wale wenye mahitaji maalum kushiriki katika maonesho haya ya 133,” inasema taarifa ya TanTrade.

Taarifa hiyo inasema mwisho wa kuthibitisha ushiriki ni Aprili 10, 2023.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter