Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Zitto ataka mwendokasi itumie gesi asilia

Zitto ataka mwendokasi itumie gesi asilia

0 comment 71 views

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Zitto Kabwe ameitaka DART kuingia mkataba mara moja na TPDC kubadilisha Mabasi ya Mwendokasi kutoka kutumia Diseli na kutumia gesi asilia (CNG).
Kabwe amesema hayo baada ya chama hicho kuichambua ripoti ya CAG.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kabwe amesema “katika Ripoti ya Mwaka 2021/2022, CAG ametoa hoja mbili kubwa za ukaguzi kuhusu Mradi wa Ujenzi wa miundombinu ya Mabasi ya Mwendokasi Dar es Salaam (DART); ujenzi kutokidhi ubora wa viwango na matumizi ya dizeli badala ya gesi kwenye mabasi ya mradi huo”

“Kuhusu eneo la dizeli, CAG amebaini kuwa TPDC imeingia gharama ya ujenzi wa miundombinu kujaza gesi asilia kwenye mabasi ya mwendokasi bila ya kuwa na mkataba na DART.”

Kwa mujibu wa CAG, DART waligoma kuingia mkataba na TPDC kwa ajili ya kubadilisha magari kutoka mfumo wa mafuta kwenda gesi kwa madai kuwa wameingia mkataba wa miaka 12 na kampuni ya kuuza mafuta ya dizeli”

“Hoja hii ya mkataba wa miaka 12 haina mashiko na ni kichaka cha ubadhirifu, taarifa tulizonazo zinaonesha kwamba DART wanatumia wastani wa lita 30,000 za diseli kuendesha huduma ya usafiri kwa siku, hii ni sawa na kutumia Shilingi milioni 91 kila siku, sawa na shilingi bilioni 33 kwa mwaka mzima.”

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter