Home Elimu Afrika Mashariki yatakiwa kuendeleza Kiswahili

Afrika Mashariki yatakiwa kuendeleza Kiswahili

0 comment 87 views

Wito umetolewa kwa nchi za Afrika Mashariki kuendeleza matumizi ya kiswahili katika maeneo muhimu ya kiutawala na kijamii.
Rais mstaafu wa Msumbiji Joaquim Chissano ametoa wito huo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utoaji Tuzo ya Taifa ya Mwl. Nyerere ya Uandishi Bunifu.

Ameeleza kuwa kiswahili ni tunu na utambulisho wa afrika na mwafrika.

Akiongelea kuhusu tuzo hizo Chissano amesema Juhudi za kutambua mchango wa wadau wa maandiko bunifu kwa lugha ya kiswahili ni muhimu na kwamba juhudi hizi ziendelezwe kwani uhai wa lugha yoyote duniani ni kuwapo na machapisho yaliyoandikwa kwa lugha hiyo.

“Ni wazi Mwl. Nyerere kwa dhati kabisa aliikuza lugha ya kiswahili kwa kuandika maandiko bunifu kama riwaya, mashairi na kutafsiri kazi mbalimbali za fasihi ya kingereza katika kiswahili hivyo ni heshima kubwa tuzo hii kupewa jina lake,”amesema Rais Chissano.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter