Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Kampuni za India kushiriki Sabasaba 2023

Kampuni za India kushiriki Sabasaba 2023

0 comment 67 views

Ubalozi wa India nchini Tanzania umeendelea na maandalizi ya kuratibu washiriki kutoka nchini India katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (DITF) ya 47.

Afisa Ubalozi wa India Nchini Tanzania Narender Kumar amesema mpaka sasa makampuni 35 kutoka Jimbo la Haryana yamethibitisha kushiriki.

Narender amesema kuwa Makampuni hayo pia yatapenda kupata wabia wa biashara katika sekta za uvuvi, kilimo, madini, afya, elimu na miundombinu.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Biashara TanTrade Fortunatus Mhambe ameushukuru Ubalozi wa India nchini Tanzania na kusema kuwa TanTrade imejianda na ipo tayari kuwahudumia washiriki wa kampuni hizo, na pia itaendelea na uratibu kuhakikisha kuwa ushiriki wao unakuwa wenye tija.

Maonesho hayo maarufu Sabasaba yanatarajiwa kuanza Juni 28 hadi Julai 13, 2023.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter