Uzalishaji wa karafuu Zanzibar umepungua kutoka tani 7,840 mwaka 2021 hadi tani 4,734 kwa mwaka 2022.
Akizungumza katika Bunge la Wawakilishi, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Visiwani humo Shamata Shaame Khamis amesema upungufu huo ni sawa na asilimia 40.
Zao la karafuu ambalo ndio zao kuu Zanzibar linachangia kwa asilimia 22.9 ya pato la Taifa visiwani humo.