Home KILIMOKILIMO BIASHARA Wakulima wapewa mafunzo sumukuvu

Wakulima wapewa mafunzo sumukuvu

0 comment 78 views

Wakulima wilayani Kiteto mkoa wa Manyara wamepewa mafunzo juu ya Sumukuvu na madhara yake.

Mafunzo hayo, yametolewa na Wizara ya Kilimo kupitia Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC).

Elimu hiyo imetolewa kwa wahanga wa madhara ya sumukuvu ambapo imelenga uvunaji, ukaushaji na uhifadhi wa nafaka kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo ili kuepusha chakula kisichafuliwe na sumukuvu.

Mradi wa TANIPAC ulianza rasmi mwaka 2019 na unatekelezwa katika halmashauri 18 kwenye mikoa kumi nchini.

Halmashauri hizo ni Itilima mkoani Simiyu, Buchosa mkoani Mwanza, Bukombe mkoani Geita, Nzega DC na Urambo mkoani Tabora pamoja na Newala na Nanyumbu mkoani Mtwara.

Halmashauri zingine ni Bahi, Chemba, Kongwa na Kondoa mkoani Dodoma pamoja na Kasulu na Kibondo mkoani Kigoma.

Mbali na hizo, TANIPAC inafanya kazi katika Halmashauri za Kiteto na Babati mkoani Manyara, Kilosa na Gairo mkoani Morogoro na Namtumbo mkoani Ruvuma.

Mradi wa TANIPAC una lengo kuu la kupunguza uchafuzi wa sumukuvu katika mnyororo wa thamani wa mazao ya chakula hususan mahindi na karanga na hivyo kuimarisha usalama wa chakula, biashara ya mazao nje ya nchi, kuimarisha afya ya jamii pamoja na kuongeza kipato cha wakulima.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter