Home KILIMO Serikali kujenga miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji

Serikali kujenga miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji

0 comment 235 views

Serikali imepanga kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa kuelekeza rasilimali zaidi kwenye ujenzi wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde wakati akizungumza kwenye mkutano wa wafanyabiashara na wadau wanaouza mazao ya kilimo ndani na nje ya nchi.

Mavunde amesema kuwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24, Serikali imeweka mkakati wa kujenga mabwawa 100 nchi nzima yenye uwezo wa kuhifadhi lita bilioni 900 nchi nzima.

Ameongeza kuwa Serikali itachimba visima 150 katika kila halmashauri kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Maeneo yenye vyanzo vya maji, hususan mito na maziwa, Serikali imepanga kujenga miundombinu itakayofikisha maji kwenye mashamba ya wakulima.

Aidha, mabonde yote nchini yatafanyiwa upembuzi yakinifu ambapo hekta 3,016,600 zitapatikana na kuwekewa miundomninu kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Ameyataja mabonde hayo kuwa bonde la ziwa Viktoria, Bugoma, Subuti, Mto Ngono, Manga Homere, Ngomai na litumbandios.

Mabonde mengine ni Mito Ruvuma, Songwe, Ifakara Idete, Rufiji ya Chini, Kilombero, Mkomazi na Pangani.

Mkutano huo umeshirikisha wafanyabiashara zaidi ya 460.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter