Home BIASHARAUWEKEZAJI Taasisi ya kifedha ya Uingereza kuwekeza Tanzania

Taasisi ya kifedha ya Uingereza kuwekeza Tanzania

0 comment 107 views

Waziri wa Fedha Dkt. ameikaribisha Taasisi ya kifedha ya Uingereza inayojihusisha na uwekezaji (British International Investment) kufanya uwekezaji nchini katika sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo ya nishati.

Dkt. Nchemba ametoa wito huo alipokutana na kufanya majadiliano na ujumbe wa British International Investment, katika Ofisi ya Hazina, jijini Dar es Salaam ambapo wameangazia mambo mbalimbali ya ushirikiano wa maendeleo.

Ametaja maeneo muhimu ya uwekezaji katika sekta ya nishati ikiwa ni pamoja na usambazaji wa umeme, kuwekeza katika mafuta na gesi kwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye akiba kubwa ya hydrocarbon yenye gesi na mafuta.

Amesema kuwa maendeleo ya miundombinu hiyo ni kipaumbele kikubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania na inatarajia kuwa na matokeo makubwa na ya haraka katika kuongeza ajira na kukuza kipato.

“Maeneo mengine muhimu ambayo Serikali imeweka jitihada ni pamoja na Ushirikiano wa Umma na Binafsi (PPPs) katika sekta za uzalishaji ambazo zina jukumu muhimu katika kuendesha maendeleo endelevu nchini.

Aidha, Dkt. Nchemba ameziagiza timu za wataalam kuhakikisha zinafanya majadiliano ya kina kuhusiana na uwekezaji ambao taasisi hiyo imeonesha nia ya kufanya uwekezaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Bw. Simon Cheung, amesema Taasisi yake ipo tayari kufanya majadiliano na Serikali ya Tanzania na kuipa kipaumbele kwenye kusaidia kuwekeza katika maeneo mbalimbali.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter