Home Elimu Vijana 20 wapata ufadhili wa Rais Samia

Vijana 20 wapata ufadhili wa Rais Samia

0 comment 163 views

Chuo cha Utalii kimepongezwa kwa kupokea vijana 20 kwa ajili ya kusomea masuala ya Utalii na ukarimu kupitia ufadhili wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Mashaka Biteko wakati akifungua Kongamano la uwekezaji la Wilaya ya Pangani katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.

Biteko ameweka msisitizo kwa vijana hao 20 ambao wanatoka wilaya ya Pangani kuwa wamepata bahati ya ufadhili huo wakasome kwa nguvu na bidii, huku akiwataka kujiepusha na mambo maovu ambayo yanaweza kuwaharibia safari yao ya Masomo.

Aidha, Biteko emeipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii ikishirikiana na Taasisi zake kwa kuendelea kuzalisha fursa na mazao mapya ya Utalii hasa kwenye Wilaya ambazo zina vivutio vya Utalii.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dunstan Kitandula amesema kuwa kongamano la Utalii la Wilaya ya Pangani litaisaidia wizara kutimiza lengo la kufikia watalii milioni tano na kufikisha mapato ya Dola za Kimarekani milioni mia sita ifikapo mwaka 2025.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter