Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Dola 1000 kwa vijana kukabiliana na mabadiliko tabia nchi

Dola 1000 kwa vijana kukabiliana na mabadiliko tabia nchi

0 comment 99 views

Vijana wapatao 10 kutoka mataifa mbalimbali duniani watapatiwa kiasi cha Dola za Kimarekani 1000 kwa ajili ya kuendeleza miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi.

Haya yamebainika wakati Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula akihitimisha kongamano la Kimataifa la vijana kuhusu Mabadiliko ya Tabia nchi katika chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Kitandula ameeleza kuwa kongamano hilo linalenga kuunda kundi la vijana wanaojitolea kuleta mabadiliko katika familia zao, jamii na mataifa yao katika jitihada za kufanya dunia yetu iwe mahali bora kwa wote.

Kitandula amewaasa vijana hao kutokuogopa mipaka wanapokuwa kwenye mapambano ya kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa ni mgogoro wa kimataifa.

Ameongeza kuwa miradi hiyo inaungwa mkono na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anaongoza mapambano ya changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.

Naye, Kamishina wa Uhifadhi kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo amesema vijana hao walipata fursa ya kutembelea msitu wa Pugu Kazimzumbwi kwa ajili ya kujionea uhifadhi wa Mazingira kupitia misitu.

Aidha, vijana hao walishiriki katika zoezi la kupanda miti ya mikoko kwenye eneo la hifadhi ya mikoko Kunduchi kwa lengo la kuhifadhi mazingira.

Kongamano hilo limejumuisha vijana wapatao 500 ambapo 300 kati yao walishiriki kwa njia ya mtandao na 200 walishiriki moja kwa moja katika Chuo kikuu cha Dar es salaam.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter