Home KILIMOKILIMO UFUNDI Uingereza, Tanzania wajadili ushirikiano sekta ya kilimo

Uingereza, Tanzania wajadili ushirikiano sekta ya kilimo

0 comment 70 views

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza kwenye Sekta ya Biashara Lord Walney na kujadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano katika Sekta ya Kilimo.

Mazungumzo hayo yamefanyika Oktoba 26, 2023 katika ofisi ya Waziri Bashe, jijini Dodoma.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na maendeleo ya utafiti wa kilimo, hifadhi ya mazingira, lishe, miundombinu na rasilimali fedha kwa ajili ya kumkwamua mkulima.

Waziri Bashe ameihamasisha Serikali ya Uingereza kuelekeza rasilimali kwenye miradi itakayowawezesha wakulima moja kwa moja kiuchumi, ambapo alitoa mfano wa uwekezaji kwenye miundombinu ya umwagiliaji kama njia mojawapo ya kumsadia mkulima asiharibu mazingira kwani atakuwa na uhakika wa kulima na kuvuna katika vipindi vyote vya mwaka bila kutegemea mvua.

Aidha, Waziri Bashe amefafanua zaidi kuwa katika misimu ya kiangazi wakulima wasio na miundombinu ya umwagiliaji hufanya shughuli zinazoharibu mazingira, ikiwemo uchomaji wa mkaa kama njia mbadala ya kujipatia kipato.

Uingereza ni moja ya nchi zinazowekeza kwa wingi hapa nchini kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo Kilimo nayo ni Sekta inayofuika.

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar, Mshauri wa Ubalozi huo katika masuala ya Teknolojia ya Kilimo na Uchumi wa Buluu, Godfrey Lwakatare na Mkurugenzi wa Mazao wa Wizara ya Kilimo Nyasebwa Chimagu walihudhuria katika kikao hicho.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter