Home KILIMO Chai yote kuuzwa kwenye mnada wa Tanzania

Chai yote kuuzwa kwenye mnada wa Tanzania

0 comment 219 views

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ametoa maelekezo kwa wakulima wadogo, wakubwa na wanunuzi wote wa chai kuwa chai yote ya Tanzania haitaruhusiwa kuuzwa nje ya utaratibu wa mnada wa Tanzania.

Amesema hayo akiwa ziarani Mkoani Tanga wakati akizindua Kiwanda cha Chai Hai (Organic Tea) cha Sakare kilichopo Bungu wilayani Korogwe.

Mnada wa chai kwa mara ya kwanza ulifanyika jijini Dar es Salaam tarehe 13 Novemba 2023 ambapo kwa kipindi chote huko nyuma Chai ya Tanzania imekuwa ikiuzwa katika mnada wa Mombasa, jambo ambalo limekuwa mwiba kwa wakulima.

Chai Ya Tanzania inasifika kwa upekee wa ubora wake na kwa kutumia mnada wa Mombasa huko nyuma imekuwa haipati bei nzuri na hivyo kuwapunguzia wakulima mapato.

“Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameturuhusu kuanzisha mnada wa chai, ametupatia fedha na kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo Serikali itajenga viwanda vingine vitano vya kuchakata chai na kukipanua zaidi kiwanda cha Sakare ili kiweze kuchakata chai nyeusi.

Serikali inalenga kuwasaidia wakulima wadogo na kuwapa nafasi wakulima wakubwa kuwa na wigo wa kuzalisha zaidi katika mashamba yao,” ameeleza Waziri Bashe.

Amewapongeza wadau wa maendeleo na watumishi kwa juhudi za kufanikisha mnada huo.

Amefafanua zaidi kuwa Serikali haitaruhusu uingizwaji wa chai ghafi kutoka nje ya nchi ikiwemo orthodox tea mbayo kwa miaka yote imekua ikiingizwa kutoka Rwanda.

Lengo la Serikali ni kulinda wakulima wa chai ndani ya nchi kwa kuhakikisha kuwa chai yao inapata soko na bei nzuri nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter