Home KILIMOKILIMO UFUNDI Katibu Mkuu Mweli asisitiza utekelezaji wa mapendekezo ya tafiti

Katibu Mkuu Mweli asisitiza utekelezaji wa mapendekezo ya tafiti

0 comment 307 views

Wadau wa Ushirika wametakiwa kuwa na mpango wa utekelezaji wa mapendekezo ya tafiti za ushrika kwa kuwashirikisha wadau wengine ili kuwe na matokeo chanya kwenye maendeleo ya ushirika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli amesema hayo wakati akifungua Kongamano la tatu la tafiti na maendeleo ya ushirika lililofanyika jijini Dodoma, Mei 28, 2024.

Katibu Mkuu Mweli ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa watafiti wa ushirika kufanya tafiti zitakazojibu changamoto za ushirika, hususan kupitia Mfuko wa Utafiti wa Ushirika.

Mweli amesema ni vizuri kukiwa na mfumo wa wazi wa madaraja ya vyama vya ushirika ambapo kila chama kitakachofanya vizuri kitapongezwa na chama kitakachofanya vibaya uongozi wake utawajibishwa kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli.

Aidha, Katibu Mkuu Mweli ameiagiza Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) kushirikiana na wadau wa ushirika ikiwa ni pamoja na kufuatilia na kuwajengea uwezo watendaji wote wa vyama vya ushirika.

Kwa upande wake, Mrajisi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege amesema maelekezo yatafanyiwa kazi huku akiongeza kuwa mwelekeo wa sasa kwenye ushirika ni kuboresha shughuli za ushirika kutoka kutoa huduma pekee na kujiendesha kibiashara.

Dkt. Ndiege ameongeza zaidi kuwa miongoni mwa vipaumbele ni pamoja na matumizi ya mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye usimamizi wa vyama vya ushirika.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter