Home KILIMOKILIMO UFUNDI Tanzania, Norway wajadili kilimo

Tanzania, Norway wajadili kilimo

0 comment 142 views

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania Tine Tonnes kuhusu ushirikiano katika maendeleo ya kilimo.

Mazungumzo hayo yamefanyika Januari 31, 2023 ambapo miongoni mwa mambo waliyozungumza ni pamoja na afya ya udongo, teknolojia za kisasa za kilimo, kilimo himilivu, mabadiliko ya tabia nchi na mbolea.

Waziri Bashe amemueleza Balozi Tonnes kuwa ili kumuwezesha mkulima asifikirie uharibifu wa mazingira kama njia mbadala ya kujikwamua kiuchumi, ni kumwezesha kuwa na miundombinu ya umwagiliaji ili aweze kulima mwaka mzima.

Viongozi hao pia wamegusia suala la uzalishaji wa mbegu na ushirikishwaji wa sekta binafsi katika kilimo, hususan kupatiwa ardhi kwa ajili ya kuongeza uzalishaji.
Waziri Bashe amemueleza Balozi Tonnes kuwa mwelekeo wa Serikali ni kuleta mageuzi katika Sekta ya Kilimo kwa kuzifanya shughuli za kilimo kama biashara rasmi huku akisisitiza umuhimu wa wadau wa maendeleo kuandaa na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa pamoja kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali.

Amesema ni vema wadau wa maendeleo kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kwa pamoja kusaidia uelekezwaji sahihi wa rasilimali kwa jamii, miradi na maeneo ili kuepuka kuwekeza sehemu moja au kurudia kazi.

Balozi Tonnes aliambatana na washauri wawili kutoka Ubalozi wa Norway ambao ni Dkt. Yassin Mkwizu, Mshauri Mwandamizi wa Kilimo, Mazingira na Utafiti pamoja na Bi. Karen-Emilie Asla, Mshauri wa Biashara na Sekta Binafsi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter