Home BIASHARAUWEKEZAJI Tsh bilioni 23.4 kujenga Soko Kuu Mwanza

Tsh bilioni 23.4 kujenga Soko Kuu Mwanza

0 comment 8 views

Shilingi bilioni 23.4 zinatumika katika mradi wa ujenzi wa Soko Kuu la jijini Mwnza ambão utakapo kamilika, utawezesha wafanyabiashara wapatao 1,400 kupata maeneo mazuri ya kufanyia biashara.

Mradi huo utakuwa na Maduka 514 (madogo, ya kati na makubwa) ndani na nje ya jengo, Vizimba 332 vya matunda na mbogamboga, Vizimba 372 vya nafaka, mama lishe maeneo 12, eneo kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo (machinga 167).

Nyingine ni ofisi tano, eneo moja la kukusanyia taka, eneo la maegesho ya magari madogo 192 chini ya usawa wa ardhi (basement) na vyoo.

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba ametembelea mradi huo ambapo ameelezwa kuwa mradi huo utasaidia kuongeza mapato ya Halmashauri ya Jiji ambapo jumla ya Shillingi Billion 3.5 zinatarajiwa kukusanywa kwa mwaka, kupendezesha Jiji na kulifanya kuwa la kisasa zaidi.

Waziri wa Fedha Dkt. mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa Mwanza.

Pia mradi huo utasaidia kukua kwa biashara nyingine kutoka kwa wafanyabiashara wa ndani, mikoa ya jirani na nje ya nchi. Mradi huu umetoa ajira kwa vijana wapatao 175 ambao walikuwa wakiendelea na kazi mbalimbali za ujenzi.

Dkt. Nchemba yuko katika ziara ya kikazi ya siku saba mkoani Mwanza, ambapo anaungana na Mawaziri wenzake wa sekta mbalimbali wanaotembelea maeneo mbalimbali ya nchi kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika mikoa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter