Home About Us

About Us

by pesatuAdmin

PESA TU ( Tovuti namba moja ya biashara)

PESA TU

Ni tovuti  inayotoa nafasi kwa watu kupata taarifa kuhusu mambo mbalimbali ya  uchumi ikiwemo biashara, viwanda, fedha na kilimo kutoka Tanzania na Afrika Mashariki. Pia utapata fursa yakujifunza kuhusu masuala ya ujasiriamali, hisa, uwekezaji na kilimo ufundi. Kupitia tovuti  hii utaweza kuona matangazo mbalimbali ya ajira.

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

KUHUSU KAMPUNI

Website hii inamilikiwa na kampuni ya Mediapix Limited. MediaPix ni kampuni ya kimataifa inayohusika na musuala ya mawasiliano, matangazo na mahusiano ya umma katika bara la Afrika na Asia. Tunatoa huduma ya ushauri wa masoko kwa sekta binafsi, taasisi za serikali, asasi zisizo za kiserikali na mashirika ya kimataifa.Pia inahusika na usambazaji wa gazeti la kingereza la “The Exchange”linalotoka kila mwezi na linahusika zaidi na mambo ya uchumi katika nchi 5 za Afrika Mashariki.

WALENGWA

PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LENGO

Kuongeza uelewa na kufahamisha watanzania mambo mbalimbali ya uchumi na uwekezaji yanayoendelea Tanzania na nchi za jirani.

MATARAJIO

Kuwa tovuti ya mambo ya uchumi inayosomwa zaidi nakutumika kama chanzo cha habari kwenye vyombo vya habari vingine Tanzania.

MAKUSUDIO

  • Kuwapatia wasomaji habari za uchumi zenye uhakika kutoka Tanzania na nchi za jirani kwa haraka punde zinapotokea.
  • Kuongeza uwelewa kwa kutoa elimu ya maswala mbalimbali ya uchumi ikiwemo uwekezaji na hisa kwa watanzania.
  • Kuwapatia taarifa watanzania kuhusu mwenendo na maendeleo ya uchumi wa nchi.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter