Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) linatarajia kutangaza gawio kubwa kwa wanahisa wake kufuatia kufanya vizuri kwa kampuni hio baada ya kujiunga na kuuza hisa zake zenyewe kwenye soko hilo.
Wachambuzi wa masuala ya hisa wanasema DSE ipo katika nafasi nzuri kutangaza gawio kubwa kwa wanahisa wake kufuatia kufanya vizuri kimapato kwa miaka miwili sasa tangu ijiunge na soko.
Taarifa za fedha ya kampuni hiyo zimeonyesha kuwa ada ya kujiunga na soko inayotozwa kwa makampuni yanayotaka kujiunga imekuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa DSE. Ada hiyo imechangia asilimia 41 ya mapato kuanzia Januari hadi Aprili 2018 and kuchangia wastani wa asilimia 36 kwa miaka miwili iliyopita.
Imeelezwa pia kuwa faida zitokanazo na uwekezaji ndio chanzo cha pili cha mapato kwa kampuni hiyo. DSE ilitangaza faida ya asilimia 40 kwa miaka miwili na pia ilionyesha kuwa na fedha za kutosha za kujiendesha.
DSE inatarajia mwenendo mzuri wa biashara na hivvo kutangaza gawio kubwa kwa wanahisa wake. Gawio la mwisho lilitolewa oktoba mwaka jana na la nyuma lilikua Machi 2017 na Julai 2016 katika kipindi cha miezi tisa kwa kiasi cha Sh. 42 kwa hisa moja.