Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIBIASHARA Museveni aliza watengeneza plastiki

Museveni aliza watengeneza plastiki

0 comment 98 views

Rais wa Uganda  Yoweri Museveni ameamuru wakuu wa usalama wa nchi hiyo kutekeleza agizo la kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki nchini humo. Rais Museveni ametoa agizo hilo wakati wa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani na kuamuru zaidi ya wazalishaji 45 wa bidhaa hizo kuacha kufanya hivyo mara moja.

Kiongozi huyo ameagiza viwanda vinavyozalisha bidhaa hizo kutengeneza, kusambaza na kuuza plastiki zenye ubora ulioruhusiwa na kusema kuwa uzalishaji wa bidhaa zilizopigwa marufuku lazima ukomeshwe.

Uganda inakuwa nchi ya tatu kwa Afrika Mashariki kupiga marufuku matumizi, uuzaji, na utengenezaji wa mifuko ya plastiki. Kenya ilipiga marufuku mifuko ya plastiki mwaka 2017 wakati Rwanda ilipitisha amri kwa nguvu kwa miaka kadhaa iliyopita.

Rais Museveni aliongeza kwa kusema kuwa , sheria ya mwaka 2010 juu ya matumizi ya magunia na mifuko ya ethene  na plastiki kabla haijaondolewa, inapaswa kutekelezwa.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyotolewa Jumanne imeshauri serikali kuzingatia kupiga marufuku au kuweka kodi nzito kwa wazalishaji wa mifuko ya plastiki kama njia mojawapo ya kupambana na ongezeko la uchafuzi wa mazingira duniani.

Makampuni ya kutengeneza mifuko hiyo nchini Uganda yamelalamikia agizo hilo na kudai kuwa kuidhinishwa kwa marufuku bila ya kuwepo kwa matumizi mbadala kunawaweka katika hali mbaya kibiashara.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter