Home VIWANDAMIUNDOMBINU MV Mwanza kuanza kazi Julai

MV Mwanza kuanza kazi Julai

0 comment 125 views

Baada ya ujenzi wake kukamilika, hatimaye kivuko kipya cha MV Mwanza kimeingia majini kwa mara ya kwanza kwa ajili ya majaribio. Wakati wa zoezi la kushusha kivuko hicho kwenye maji, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Vivuko wa Wakala wa Umeme na Ufundi (Temesa), Kokombe King’ombe ameeleza kuwa kivuko hicho ambacho kinatarajia kufanya safari kati ya Kigongo na Busisi kimetengenezwa kisasa na kitakuwa na kasi zaidi kuliko vile vitatu vilivyopo hivi sasa.

Kivuko cha MV Mwanza kimejengwa na kampuni ya Songoro Marine ya jijini humo na kimegharimu takribani Sh. 8.9 bilioni. Kivuko hicho kinatazamiwa kubeba abiria zaidi ya 1000 pamoja na magari 36. Vilevile, inatarajiwa kuwa kivuko hicho kitasafirisha abiria kukota mkoani Mwanza kuelekea Geita, Kigoma, Kagera na nchi jirani za Burundi, Rwanda na Congo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Songoro Marine Salehe Songoro amesema kivuko hicho tayari kimekamilika lakini kwa kipindi cha wiki tatu, kitakuwa kwenye majaribio. Songoro ameongeza kuwa kivuko hicho kitaanza kazi rasmi mwezi Julai na kitavusha abiria kutoka Kingongo kwenda Busisi wilayani Sengerema.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter