Home BIASHARAUWEKEZAJI TTCL yamwaga manoti serikalini

TTCL yamwaga manoti serikalini

0 comment 112 views

Shirika la mawasiliano Tanzania (TTCL) limetoa gawio kwa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania la kiasi cha shilingi 1.5 bilioni kutokana na kutengeneza faida ya shilingi 28.5 bilioni kwa mwaka jana.

Shirika hilo lilipata faida ya bilioni 29.2 kwa kufanya biashara kwa mwaka jana kabla ya kukatwa kodi na kubaki na bilioni 28.5

Pia mtendaji mkuu wa shirika hilo Waziri kindamba alibainisha mbele ya raisi magufuli na waziri mkuu kassim majaliwa aliyekua anafatilia hafla hiyo kupitia mtandao wakati wa makabidhiano ya hundi hiyo kuwa faida hiyo imetokana na kubana matumizi hasa kupunguza safari za nje na kuepuka mikataba mibovu pamoja na kuongezeka kwa ufanisi wa kiutendaji kwa wafanyakazi wa shirika hilo.

Shirika hilo la mawasiliano lilianzishwa na sheria ya bunge ya mwaka 1993 na lilianza rasmi operasheni zake januari 1 1993 na baadaye mwaka 2011 lilibinafsishwa kwa wawekezaji wa kigeni walionunua asilimia 35 ya hisa kabla ya serikali kuamua kulirejesha rasmi mikononi mwake ambapo mchakato ulikamilika februari 2018 na sasa ni mali ya serikali.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter