Home VIWANDAMIUNDOMBINU Watumiaji wa daraja la Kigamboni kuendelea kulipa

Watumiaji wa daraja la Kigamboni kuendelea kulipa

0 comment 130 views

Serikali imetangaza kuendelea kuwatoza watumiaji wa daraja la Kigamboni na kusema kuwa ni sehemu mojawapo ya uwekezaji wa Shirika la taifa hidahi ya jamii (NSSF). Hayo yameelezwa bungeni Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Antony Mavunde alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Zainab Mndolwa Amir.

Mavunde amedai NSSF inategemea mapato yanayotokana na daraja la Kigamboni ili kuendesha shughuli zake mbalimbali ikiwemo kulipia mafao ya wanachama.

Mbali na maelezo hayo, Mavunde amelitaarifu bunge kuwa hadi kufikia Machi mwaka huu, tayari zaidi ya Sh. 19 bilioni zimekusanywa tangu daraja hilo lianze kutumika rasmi Mei 2016

Kwa mujibu wa maelezo ya Naibu huyo, hibi sasa serikali ipo katika mchakato wa kuweka utaratibu wa matumizi ya kadi maalum na kwamba serikali inatafuta mkandarasi wa kuweka mfumo huo wa malipo ambao utawezesha watumiaji kulipia kwa siku, wiki au mwezi kulingana na uwezo wao.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter