Home VIWANDAMIUNDOMBINU Makandarasi wanaozembea kuchukuliwa hatua

Makandarasi wanaozembea kuchukuliwa hatua

0 comment 123 views

Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani amewataka viongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kuwachukulia hatua kali za kisheria makandarasi wote katika mradi wa REA III walioshindwa kufikia kiwango cha utekelezaji wa miradi kulingana na mkataba.

Dk. Kalemani amesema hayo alipokuwa katika kikao na viongozi wa juu wa TANESCO, Wakala wa REA, Makandarasi pamoja na wazalishaji wa vifaa vya umeme walio na mikataba na miradi ya umeme vijijini.

Waziri Kalemani ameongeza kuwa, serikali haitovumilia mkandarasi yoyote aliyechukua fedha na kushindwa kutekeleza miradi hiyo ifikapo Juni 2019.

Kwa upande wao, wazalishaji katika miradi hiyo wamesema wanadhamiria kuzalisha kwa kiwango cha juu ili kuunga mkono serikali na azma yake ya kusambaza umeme kwa wananchi waishio vijijini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter