Home VIWANDAMIUNDOMBINU Prof. Mbarawa aipongeza Dawasa

Prof. Mbarawa aipongeza Dawasa

0 comment 108 views

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (Dawasa) kwa kuratibu mradi wa aina yake wa maji katika kambi ya mradi mkubwa wa umeme wa Stiegler’s Gorge. Akiwa katika eneo la mradi huo, Prof. Mbarawa amedai mradi huo wa maji utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita 209,000 ambazo zitatumika katika kambi ya ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya Mto Rufiji.

Waziri huyo amefafanua kuwa kupitia mradi huo wa maji, wakandarasi katika bwawa la kufua umeme sasa wataendesha shughuli zao kwa ufanisi zaidi kutokana na kuwa na uhakika wa maji wakati wote.

“Miundombinu wezeshi itawapa fursa wakandarasi wafanye kazi kwa ufanisi mkubwa kwasababu maji yatakuwa yanapatikana muda wote na kila siku na hili litasaidia katika kuhakikisha mradi wetu wa ujenzi wa bwawa la umeme kumalizika kwa muda uliopangwa.” Amesema Prof. Mbarawa.

Akizungumzia mradi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Dawasa Dk. Suphian Masasi amesema taifa zima litanufaika nao kwani upatikanaji wa maji ya uhakika utasaidia wakandarasi kuendesha shughuli zao. Dk. Masasi pia ameweka wazi kuwa walifanya marekebisho kwenye baadhi ya miundombinu chakavu kabla ya kuanza usambazaji wa maji hayo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter