Home VIWANDAUZALISHAJI JPM awatafutia soko wakulima

JPM awatafutia soko wakulima

0 comment 25 views

Rais John Magufuli amewashauri mabalozi  wa nchi ambazo zinakumbwa na uhaba wa chakula kununua hapa nchini ili kuwawezesha wakulima kupata masoko. Rais Magufuli amesema hayo Ikulu jijini Dar es salaam alipokuwa anakabidhi hati za utambulisho za viwanja kwa mabalozi pamoja na mashirika ya kimataifa yenye makazi yake nchini kwa ajili ya kujenga ofisi na makazi Dodoma ambapo hati 67 zimekabidhiwa na kati ya hizo, 62 ni za balozi za nchi huku tano zikiwa za mashirika ya kimataifa.

Rais ameeleza kuwa serikali inafanya jitihada za kutafuta soko kwa ajili ya chakula ili kutowavunja moyo wakulima ambao wamezalisha ziada msimu huu huku nchi ikiwa imejitosheleza na chakula.

“Kama kuna chakula kinatakiwa kupelekwa kwa refugees (wakimbizi), kwa nini mkanunue chakula kutoka nje huko Ulaya na kukisafirisha kwa gharama kubwa, si chukua hapa tu Songea”. Amesema Rais Magufuli.

Pamoja na yote hayo, Rais Magufuli pia amesema tayari amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) David Beasley ambaye amejionea ziada ya chakula iliyopo nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter