Home BIASHARAUWEKEZAJI Uwekezaji wa China kuinufaisha Zanzibar

Uwekezaji wa China kuinufaisha Zanzibar

0 comment 185 views

Serikali ya China na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wametiliana saini ya makubaliano kuhusu namna ya kuhifadhi maeneo ya kihistoria kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya utalii visiwani humo. Akizungumza mjini Zanzibar Katibu Mkuu wa wizara ya habari, utalii na mambo ya kale, Khadija Bakari Juma  amesema makubaliano hayo ni dalili njema na uthibitisho wa umoja,ushirikiano,uhusiano na mshikamano uliopo kati ya nchi hizo mbili na kuongeza kuwa utasaidia kuvitangaza zaidi vivutio na maeneo ya kihistoria kama fursa mojawapo ya utalii inayopatikana katika visiwa hivyo.

“Utiaji saini huu utaweka misingi bora ya kusaidiana na kuhakikisha maeneo ya kihistoria yaliyopo yanarejeshwa hadhi yake kwa kufanyiwa matengenezo kama itakavyoonekana inafaa kwa maslahi ya jamii” Amesema Khadija.

Aidha mkataba huo umenuia katika kubadilishana uzoefu baina ya serikali hizo mbili katika namna ya utunzaji wa maeneo ya kihistoria pamoja na makumbusho ili vivutio hivyo vizidi kutunzwa na kuwepo kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Kwa upande wake Waziri wa mambo ya kale wa China, Liu Yuzhu amesema uhusiano mzuri baina ya serikali hizo mbili ndio uliopelekea makubaliano ya mkataba huo na kudai kuwa, China itaendelea kushirikiana na Zanzibar katika kuiinua sekta ya utalii kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter