Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI SIDO kutoa huduma kwa mtandao

SIDO kutoa huduma kwa mtandao

0 comment 146 views

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo nchini (SIDO) Prof. Sylvester Mpanduji amesema shirika hilo linatarajia kutengeneza mfumo wa kielektroniki wa taarifa zake nchi nzima. Prof. Mpanduji ameeleza kuwa tayari Sh. 1.5 bilioni imetengwa kwa ajili ya mfumo huo unaolenga kurahisisha utoaji huduma kwa wajasiriamali pamoja na utendaji kazi.

“Lengo letu ni kutoa huduma bora kwa wajasiriamali ili kukuza sekta ya viwanda na biashara nchini hatimaye kufikia azma ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025”. Amesema Mkurugenzi huyo.

Kwa mujibu wa Prof. Mpanduji, SIDO inafanya jitihada za kutoa mafunzo, elimu pamoja na mitaji kwa wajasiriamali na mfumo huo utakaotengenezwa utasaidia kuweka taarifa muhimu na kumbukumbu za wajasiriamali, hivyo kurahisisha ufuatiliaji wa maendeleo.

Mbali na maandalizi ya mfumo huo wa kielektroniki, Prof. Mpanduji pia amezungumzia jitihada za shirika hilo katika kuendeleza nguvu kazi na uwezo ili kutengeneza mazingira rafiki ya biashara na viwanda na shughuli nyingine kufanywa katika misingi ambayo ni rahisi kufuatilia na kuona maendeleo. Mkurugenzi huyo pia ameongelea kuhusu mchango mkubwa wa Tehama katika kuboresha shughuli za ujasiriamali.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter