Wanawake ni kundi lenye mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa lolote. Mara nyingi kundi limekuwa likiachwa nyuma, suala ambalo limepelekea mchango wao wa moja kwa moja usionekane. Ili kubadili mtazamo huu, jamii inapaswa kubadilika ili kuwe na mazingira ambayo yatahamasisha wanawake kujituma zaidi na kufikia malengo yao.
Ni vizuri kwa taifa kuwa na mikakati ambayo ikizingatiwa itasaidia kuinua wanawake na kuwapa nafasi ya kuonyesha mchango wao katika jamii. Zifuatazo ni baadhi tu ya vipengele ambayo vinaweza kusaidia kufanikisha azma hii:
- Kutoa nafasi zaidi za uongozi
- Jamii kuungana na kupiga vita mfumo dume
- Kuweka mazingira ya wanawake kujitegemea
- Wanawake washirikishwe zaidi katika harakati za maendeleo
- Kupiga vita ubaguzi wa kijinsia
- Upatikanaji rahisi wa mikopo
- Uwekezaji zaidi katika shughuli za wanawake
- Kuwa na sera zitakazolinda wanawake
- Watoto wa kike wapatiwe elimu
- Serikali iendelee kusaidia vikundi vidogo vya wanawake wajasiriamali
- Kuwapa nafasi wanawake kuwa wabunifu
- Kuandaa matamasha ya wanawake kujadiliana na kubadilishana mawazo
- Kutatua changamoto zinazowarudisha nyuma wanawake
Kundi hili lina umuhimu mkubwa katika harakati za maendeleo na ni jukumu la jamii nzima kuhakikisha kuwa, kuna mazingira rafiki kwa ajili yao. Kuelekea Tanzania ya viwanda, wanawake wasiachwe nyuma na badala yake washirikishwe kikamilifu katika ujenzi wa taifa.