Home VIWANDAUZALISHAJI Dangote kuanza kutumia gesi asilia

Dangote kuanza kutumia gesi asilia

0 comment 117 views

Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani amesema serikali ya awamu ya tano imedhamiria kumuwezesha kila mwananchi kufikia uchumi mkubwa ikizingatiwa kuwa nchi inaelekea kwenye uchumi wa viwanda. Dk. Kalemani amesema hayo wakati akizindua mradi wa kuunganisha miundombinu ya gesi asilia kwa kiwanda cha saruji cha Dangote, mradi ambao utawezesha uzalishaji mkubwa kufanyika na kushusha bei ya saruji.

“Kubwa niwaombe wananchi kutunza miundombinu yetu ili iweze kudumu na iweze kutusaidia kukuza uchumi wetu”. Amesema Dk. Kalemani.

Akizungumza katika uzinduzi huo,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Emmanuel Gilbert amesema mradi huo unatazamiwa kusafirisha takribani futi za ujazo 30 milioni za gesi asilia kwa siku, kiasi ambacho kitatumika kuendesha mitambo ya kuzalishia saruji itakapofika Novemba mwaka huu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Dangote, Jagat Rathee amesema matumizi ya gesi asilia yatashusha gharama za uzalishaji wa saruji kwa kiasi kikubwa na pia itachochea kiwanda hicho kuzalisha bidhaa zaidi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter