Home BIASHARA Mifumo dhabiti muhimu kwa mashirika ya umma

Mifumo dhabiti muhimu kwa mashirika ya umma

0 comment 26 views

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta Tanzania (TPB) Dk. Edmund Mndolwa ametaja sababu ya mashirika mengi ya umma kutofika mbali kuwa ni kukosa mfumo dhabiti wa kiuongozi unaowaongoza kufanya vizuri. Dk. Mndolwa amesema hayo katika mkutano wa kimataifa wa mwaka ulioandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa Mahesabu ya Ndani nchini (IIA) ambapo ameongeza kuwa mashirika zaidi ya 400 yamekufa kutokana na kukosa mfumo sahihi.

“Huwezi kupuuza mfumo wa kiuongozi katika kuendesha taasisi au mashirika ya umma, labda mashirika ambayo tulikuwa nayo zamani yangeendelea kama kungekuwa na mfumo imara wa kiuongozi wenye nia moja ya kuendesha mashirika hayo”. Amesema Mwenyekiti huyo.

Katika maelezo yake, Dk. Mndolwa amesema kuna kila sababu ya kubadili mfumo wa kuendesha na kuongoza mashirika hasa katika usimamizi na kutoa mfano wa kampuni ya Enron Corporation ya Marekani iliyotangazwa kufilisika mwaka 20001 kwa kukosa kuwa na uongozi thabiti wa mfumo wa uendeshaji wake.

“Huu mfumo wa uongozi wa mashirika ni kitu kinachotakiwa kuwa akilini mwetu muda wote na kufanyiwa tathmini ya mara kwa mara ili mashirika ya umma yaweze kuendelea”. Ameeleza Dk. Mndolwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter