Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI JPM: Serikali itaendelea kumuenzi Nyerere kwa vitendo

JPM: Serikali itaendelea kumuenzi Nyerere kwa vitendo

0 comment 114 views

Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli amesema serikali itaendelea kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere kwa kuhakikisha fikra na mipango mizuri aliyoweka inatekelezwa kwa manufaa ya taifa letu. Rais Magufuli amesema hayo jana, Oktoba 14 wakati akizungumza na mjane wa Mwalimu, Mama Maria Nyerere jijini Dar es Salaam alipokwenda kumtembelea mara baada ya kushiriki misa takatifu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Rais Magufuli amenukuliwa akisema kuwa, Mwalimu Nyerere alifanya kazi kubwa ya kujenga misingi bora na imara ya nchi kuwa na amani, umoja na mshikamano na vilevile kujenga misingi ya uchumi wa kujitegemea kupitia Azimio la Arusha.

Pamoja na hayo, Rais Magufuli ambaye aliongozana na mkewe, Janeth Magufuli pia ametoa wito kwa watanzania wote hususani vijana kuungana na kushirikiana kikamilifu na serikali katika kuyaenzi yale yaliyofanywa na Mwalimu Nyerere na pia kuliombea taifa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter