Home KILIMO Wakulima wa pareto washauriwa kujiunga ushirika

Wakulima wa pareto washauriwa kujiunga ushirika

0 comment 74 views

Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba ametoa wito kwa wakulima wa pareto nchini kujiunga na mfumo rasmi wa vyama vya msingi vya ushirika kwani ni dhana ianyolenga kuleta maendeleo na imeonyesha mafanikio kiuchumi pamoja na kijamii katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita. Dk. Tizeba amesema hayo wakati akizungumza na wakulima wa pareto katika kijiji cha Ikanga wilayani Mufindi ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kikazi mkoani Iringa.

“Kutokana na changamoto mbalimbali zilizoikumba sekta hii ya ushirika watu wengi wamekosa imani na vyama hivi na baadhi ya vyama vimeshindwa kufanya kazi vizuri hivyo nawahakikishia serikali inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli imerejesha nidhamu kwenye ushirika” Aidha, Waziri Tizeba amefafanua kuwa, maana halisi ya ushirika ni muungano wa watu wanaofanya kazi pamoja kwa hiari ili kufanikisha mahitaji yao ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kupitia shughuli ya biashara inayomilikiwa kwa pamoja na kudhibitiwa kidemokrasia huku maadili ya kujisaidia wenyewe, jukumu binafsi, demokrasia, usawa na mshikamano yakizingatiwa.

Waziri Tizeba amewataka wakulima wanaofanya kilimo hicho katika mikoa ya nyanda za juu kusini na maeneo yote nchini kwa ujumla kulima zao hilo kwa wingi ili wapate fursa ya kuinua kipato chao na kupiga vita umaskini kutokana na kuwepo kwa soko la uhakika la zao hilo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter