Home BIASHARAUWEKEZAJI AfDB yasaka fursa za uwekezaji Mbeya

AfDB yasaka fursa za uwekezaji Mbeya

0 comment 106 views

Wataalamu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wamewasili mkoani Mbeya wakiwa na lengo la kutazama maeneo ya kipaumbele katika uwekezaji hasa katika viwanda cya kuchakata mazao ya chakula. Wataalamu hao 15 wamepatanafasi ya kutembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe pamoja na mradi wa mbegu za viazi mviringo wa STAWISHA. Mara baada ya kuzungumza na wataalamu hao, Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema ugeni huo kutoka AfDB una nia ya kuwekeza katika mnyororo wa thamani wa mazao ya chakula ili kuchochea ajira hasa kwa vijana.

“Ziara hii ni matokeo ya mazungumzo yaliyofanywa na Rais Magufuli na Mkurugenzi Mkuu wa AfDB walipokutana nchini hivi karibuni. Benki itatoa fedha zitakazowezesha ujenzi wa maeneo ya viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo”. Ameeleza Chalamila.

Pamoja na hayo, Mkuu huyo ameongeza kuwa tayari mkoa wa Mbeya umeshatenga maeneo kwa ajili ya kujenga viwanda, kuainisha mazao ya kipaumbele ya mkoa kwa kushirikiana na SAGCOT kupitia kongani ya Mbarali inayoileta pamoja mikoa ya Songwe na Mbeya. Chalamila amesema kuwa serikali ya Rais Magufuli inalenga kuboresha maeneo yote ya uwekezaji ili kuendelea kuwavutia wawekezaji zaidi.

“Ujenzi wa miundombinu wezeshi itasaidia uwekezaji kwenye viwanda na kusaidia mazao kutoharibika au kukosa masoko”. Amesisitiza Chalamila.

Kwa upande wake, Meneja wa SAGCOT Mbarali, Tulla Mloge amesema ziara hiyo mkoani Mbeya ni kielelezo tosha cha dhamira ya serikali ya kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter