Home VIWANDAMIUNDOMBINU Mradi mkubwa wa maji wazinduliwa Mbinga

Mradi mkubwa wa maji wazinduliwa Mbinga

0 comment 146 views

Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa amezindua mradi mkubwa wa uboreshaji wa huduma ya maji mjini Mbinga mkoani Ruvuma ikiwa ni hatua ya serikali kufanikisha lengo la kufikia asilimia 90 kwa miji mikuu ya wilaya ifikapo mwaka 2020 ambapo takribani Sh. 1.2 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji kwa miji 25 Tanzania bara na visiwani. Waziri Mbarawa ameongeza kuwa, mradi huo mbali na kutoa huduma ya majisafi na majitaka kwa wananchi, pia utabadilisha maisha ya wakazi wa Mbinga kwa kiasi kikubwa kutokana na umuhimu wake katika shughuli za kila siku za kiuchumi.

Mradi huo uliopo chini ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya mji wa Mbinga (MBIUWASA) ulianza rasmi kujengwa Mei, 2017 ukigharimu Sh. 1.029 bilioni na ulianza kutoa huduma ya maji kwa mjini hapo mwezi Februari mwaka huu. Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka hiyo, Patrick Ndunguru amesema kumalizika kwa mradi huo kumepelekea ongezeko la uzalishaji wa maji kutoka wastani wa lita 700,000 kipindi cha kiangazi na lita 1,600,000 kipindi cha masika. Meneja huyo pia ameweka wazi kuwa, kukamilika kwa mradi huo pia kumechangia kuongeza mapato kutoka Sh. 18 milioni hadi Sh. 25 milioni kwa mamlaka hiyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter