Home FEDHAMIKOPO SIDO yamwaga mabilioni kwa wajasiriamali Manyara

SIDO yamwaga mabilioni kwa wajasiriamali Manyara

0 comment 116 views

Meneja wa Shirika la Viwanda Vidogo nchini (SIDO) mkoani Manyara, Abel Mapunda amesema wajasiriamali mkoani humo wamenufaika na kupata mikopo ya thamani ya Sh. 2.1 bilioni kutoka shirika hilo. Pamoja na upatikanaji wa mikopo, Mapunda ameeleza kuwa SIDO imefanikisha uanzishwaji wa viwanda vidogo vipya takribani 350 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Mapunda ameweka wazi kuwa wamefamikiwa kufanya yote hayo kutokana na ushirikiano uliopo kati ya shirika hilo na Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa wilaya, asasi binafsi pamoja na wananchi kwa ujumla.

Mbali na hayo, Meneja huyo ameeleza kuwa mkoa wa Manyara una rasilimali mbalimbali ambazo zinategemea uanzishaji wa viwanda katika teknolojia ya mashine kupitia fursa za aina tofauti zikiwemo kilimo, ufugaji na madini.

“Tunashirikana na serikali na taasisi kwa ajili ya kutoa elimu ya ujasiriamali ambayo kwa namna moja au nyingine yatasaidia jamii ikiwemo kugawa mashine”. Ameeleza Mapunda.

Kadhalika, Meneja huyo amesema SIDO itaendelea kuwaunga mkono wajasiriamali kwa kugawa mashine kwa wilaya zote za mkoa huo ili kuwajengea wajasiriamali uwezo na kuwainua kiuchumi.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter