Home BIASHARAUWEKEZAJI Dk. Kalemani: Mradi wa bomba la mafuta haujasimama

Dk. Kalemani: Mradi wa bomba la mafuta haujasimama

0 comment 118 views

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amesema utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta kutoka (Hoima) Uganda hadi Tanga haujasimama na kueleza kuwa, hatua za utekelezaji wa mradi huo bado zinaendelea. Dk. Kalemani amesema hayo jijini Dar es salaam katika mkutano uliokuwa ukijadili utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa bomba hilo uliomkutanisha Waziri huyo na Waziri wa Nishati na Madini wa Uganda, Irene Muloni.

Dk. Kalemani amefafanua kuwa, utekelezaji wa mradi huo upo katika hatua nzuri na kudai pande zote mbili zimejadiliana na kukubaliana kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati uliopangwa pamoja na hatua za utkelezaji za mradi.

“Mradi haujasimama tunaendelea na utekelezaji tumekubaliana tukamilishe ndani ya wakati tuliokubaliana pande zote mbili”. Amesema Dkt. Kalemani.

Katika maelezo yake, Waziri Kalemani amesema upande wa Tanzania tayari wamekamilisha tafiti ya tathmini ya mazingira, ustawi wa jamii pamoja ulipaji fidia  kwa wananchi mkoani Tanga.

Naye Waziri Muloni wa Uganda amesema watahakikisha watafikia makubaliano na makampuni ili kufanikisha kusaini utekelezaji wa mradi huo unaotarajiwa kumalizika mwaka 2020. Waziri huyo Amefafanua kuwa ifikapo Januari 2019, mkutano mwingine utafanyika nchini Uganda na masuala yaliyobaki yatajadiliwa ili makampuni yaanze utekelezaji mara moja.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter