Home KILIMOKILIMO BIASHARA Tanzania kuuza mahindi nje

Tanzania kuuza mahindi nje

0 comment 147 views

Wakulima wa mahindi nchini Tanzania kuanza kuuza mahindi nje ya nchi baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya kuuza mahindi baina ya wakala wa taifa wa hifadhi za chakula (NRFA) na shirika la chakula duniani (WFP).

Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo umefanyika leo ikulu jijini dar es salaam na kushuhudiwa na rais Dk John Magufuli huku pande zote mbili zikiwakilishwa viongozi wakuu.

Katika makubaliano hayo NFRA itawauzia tani za mahindi 36000 zenye thamani ya bilioni 21 huku hitaji la Wfp likiwa ni tani 45000.

Pia Rais Magufuli alipongeza NRFA kwa uamuzi huo wa kuuza mahindi kwani unawapa motisha wakulima.

“Kwa uhakika huu, ninaimani wakulima wetu wa mahindi, mtama, mpunga na kadhalika wataweza kupata ufumbuzi wa kilio chao cha bei, na tutafanya hivi kwa mazao mengi.” Amesema Rais Magufuli.

Amewataka watendaji wa miundombinu na wasimamizi wa mamlaka zinazohusika Kama vile Tanroad,TPA,TRA na jeshi la polisi kuacha urasimu na kuongeza kuwa wanachelewesha maendeleo.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter