Home FEDHAHISA Serikali kumiliki 49% hisa Airtel Tanzania

Serikali kumiliki 49% hisa Airtel Tanzania

0 comment 139 views

Kampuni ya Bharti Airtel imeridhia kuongeza hisa zinazomilikiwa na serikali katika kampuni ya Airtel Tanzania kutoka asilimia 40 hadi asilimia 49. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, serikali itamiliki asilimia 49 ya hisa za Airtel Tanzania baada ya mazungumzo kati ya Rais Magufuli na Mwenyekiti wa kampuni ya Bharti Airtel, Sunil Mittal.

Katika taarifa hiyo, imeelezwa kuwa wawili hao wamezungumzia maendeleo ya mazungumzo ya umiliki wa hisa za kampuni ya Airtel Tanzania ambapo Mittal amekubali kuongeza hisa zinazomilikiwa na serikali hivyo kufanya hisa za Bharti Airtel kushuka hadi asilimia 51 kutoka asilimia 60.

Naye Rais Magufuli ameeleza kufurahishwa na hatua iliyofikiwa katika mazungumzo hayo pamoja na ongezeko la hisa za serikali katika umiliki wa Airtel Tanzania.

“Masuala mengine ya kumalizia mazungumzo haya yataendelea leo ili kumalizia, lakini jambo zuri ni kuwa sasa wamekubali kutoa gawio kwa Serikali ambapo kwa muda wa miaka minane hadi kumi tulikuwa hatujapata gawio. Kiasi cha asilimia za gawio nacho watajadili leo, kwa hiyo mimi naona huu ni mwanga mzuri wa kwenda mbele kati ya kampuni ya Bharti Airtel na serikali ya Tanzania pamoja na kampuni zingine”. Amesema Rais Magufuli.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter