Home FEDHAMIKOPO Madeni elimu ya juu kulipwa kupitia GEPG

Madeni elimu ya juu kulipwa kupitia GEPG

0 comment 106 views

Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, (HESLB) Abdulrazack Badru amesema bodi hiyo imekuja na mfumo mpya wa kielektoniki uliyopewa jina la Goverment Electronic Payment Getway (GEGP) ambao utatumika kulipa madeni ya waliokuwa wanufaika wa mikopo.

Akitangaza mfumo huo Badru ameeleza kuwa mfumo huo utarahisisha uwazi katika ukusanyaji wa fedha hizo na kumuwezesha mdaiwa kulipa mahali popote alipo pamoja na kutoa fursa ya kuongezeka kwa mapato ya bodi hiyo.

“Tumekamilisha utaratibu mfumo wa serikali wa kukusanya mapato (GEPG), mwajiri na wanufaika watatakiwa kujiunga kwenye mfumo huu mpya wa GEPG ili kulipa madeni wanayodaiwa na serikali. Waajiri ambao watashindwa kulipa madeni ya wafanyakazi ambao walikuwa ni wanufaika, tutawaanzishia operesheni maalumu ya kupitia maofisini kwao ili kuwabaini wasiolipa mikopo ya bodi”. Amesema Badru

Akifafanua mfumo huo mpya, Mtaalamu wa GEPG, Baziri Bajunia ameeleza kuwa:

“Mfumo huu umekuwa ukitumika sasa hivi na taasisi nyingi ambazo zinafanya malipo kwa taasisi za serikali, ni utaratibu ambao hata taasisi nyingine za kifedha wanautumia”

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter