Home BIASHARA Waliosababisha hasara sokoni Kariakoo kuwajibishwa

Waliosababisha hasara sokoni Kariakoo kuwajibishwa

0 comment 27 views

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameagiza kukamatwa kwa Mkuu wa idara ya fedha, Mkuu idara ya utumishi, Mkuu idara ya manunuzi na aliyekuwa Mkuu wa idara ya mipango na biashara wa soko la kimataifa la Kariakoo kwa kuisababishia serikali hasara ya takribani Sh. 1.3 bilioni. Makonda ameagiza hayo akiwa kwenye mkutano wa utatuzi wa kero za wafanyabiashara wa soko hilo na kutoa siku tano kwa watendaji kupitia upya sheria zote za ushuru baada ya kubaini uwepo wa ushuru mkubwa, hali inayowaumiza na kuwarudisha nyuma wafanyabiashara.

“Hatuwezi kuwa na shirika linaloongeza kero kwa wafanyabiashara na kuwarudisha nyuma, haiwezekani mtu alipie kodi ya pango, ushuru wa kuingiza mzigo 600, ushuru wa siku 1,700, muuza kahawa alipe 1,000 na bado mtu huyo huyo analipa ushuru wa choo na bafu 500, hili haliwezekani” Amesema Mkuu huyo wa mkoa.

Mbali na hayo, Makonda ameagiza soko la kariakoo kurejeshwa kwenye hadhi ya kimataifa na kuvunjwa kwa mkataba wa makusanyo ya ushuru baina ya mbia na soko na badala yake kutaka kazi ya kukusanya ushuru kufanywa na uongozi wa soko.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter