Home BIASHARA Wafanyabiashara Dar wapewa mafunzo kuhusu umuhimu wa kodi

Wafanyabiashara Dar wapewa mafunzo kuhusu umuhimu wa kodi

0 comment 134 views
Na Mwandishi wetu

Kampuni ya PFK inayojihusisha na masuala ya ushauri wa kibiashara, imeanza kampeni maalum inayolenga wafanyabiashara kuelewa umuhimu wa kulipa kodi. Hatua hiyo imekuja baada ya kugundulika kwamba wafanyabiashara wengi nchini hawana elimu ya kutosha kwenye masuala ya umuhimu wa kodi.

Mara baada ya kuelimika na kufahamu umuhimu wa kulipa kodi, Bw Mustansir Gulamhussein ambaye ni mshirika wa PFK amesema kuwa, Watanzania watakubaliana na wajibu huo wa kulipa kodi zao hivvo kupelekea serikali kukusanya mapato zaidi. Mapato haya yatapelekea miradi mingine ya kimaendeleo kuendelea na kunufaisha wananchi wote kwa ujumla.

Walipa kodi wanapaswa kufahamu taratibu za ulipaji kodi, na kwamba kuna sheria zinazolinda haki zao. Mafunzo haya ni ya umuhimu mkubwa kwa wafanyabiashara kwani tangu Julai 01 mwaka huu sheria ya fedha imebadilisha miongozo na kanuni mbalimbali kuhusiana na masuala ya kodi ambayo wananchi wanapaswa kufahamu.

Lengo la mafunzo haya ni kuelimisha watanzania wengi ipasavyo na PKF imejipanga kuendesha semina hizi nchini kote, kwani wana wataalamu wenye uzoefu mkubwa katika masuala haya ya biashara na wenye uelewa mkubwa wa soko la ndani hivyo kuwafanya kuwa washauri wazuri kwa wamiliki wa biashara kote nchini.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter