Home KILIMO Makubwa yanakuja wakulima wa pamba

Makubwa yanakuja wakulima wa pamba

0 comment 108 views

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amesema Wizara hiyo imejipanga kuwakomboa wakulima wa pamba na tayari imeanzisha zoezi la usajili kwa wakulima wote nchini, ambapo serikali imetengeneza mfumo maalumu wa kuwatambua wakulima, maeneo walipo, ukubwa na mahali mashamba yao yalipo.

Waziri Hasunga ameeleza hayo jijini Dodoma wakati wa kikao maalum na wabunge kutoka maeneo yanayolima pamba na kusema kuwa, Wizara ya Kilimo inapitia upya mfumo wa ushirika katika ununuzi wa pamba, mfumo wa uagizaji na uingizaji wa viuatilifu vya pamba pamoja na masoko.

“Napenda nikiri kuwa tuna tatizo katika mfumo wa uagizaji na uingizaji wa pembejeo za kilimo, bado haujakaa vizuri lakini baya zaidi ni viuatilifu hafifu. Serikali kamwe haiwezi kutazama wakulima wakionewa na wajanja wachache na huu ni uhujumu uchumi lazima wanaofanya mambo haya wachukuliwe hatua kali za kisheria”. Amesema Waziri huyo.

Lengo kubwa la kikao hicho lilikuwa ni kufanya maboresho ili kujiandaa na msimu ujao wa mauzo ya pamba ambao unatarajia kuanza mwezi Aprili mwaka huu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter