Home KILIMO Malipo wakulima wa korosho yafikia bilioni 500

Malipo wakulima wa korosho yafikia bilioni 500

0 comment 114 views

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema zaidi ya Sh. 500 bilioni tayari zimeshalipwa kwa wakulima wa korosho huku malipo yakiwa bado yanaendelea kwa wakulima waliosalia. Majaliwa amesema hayo bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Zuberi Kuchauka, Mbunge wa Liwale aliyehoji kuhusu malipo kwa wakulima wa korosho ambao walikuwa wakilipwa Sh. 2,600 kwa kilo wakati Rais Dk. Magufuli alitangaza kuwa serikali itanunua kilo moja ya korosho kwa Sh. 3,300.

“Malipo yanaendelea na sehemu kubwa ni kwa wakulima wenye kilo zaidi ya 1,500, serikali itanunua korosho zote kama ilivyoelezwa. Taratibu zinazofanyika ni kuhakikisha anayelipwa ni muhusika. Wananchi endeleeni kuiamini serikali yenu”. Amesema Waziri Mkuu.

Majaliwa amesema serikali inapaswa kufanya uhakiki kwa wakulima, ili kujiridhisha kama ni wakulima, hivyo mara baada ya kuhakikiwa, wakulima wote watalipwa fedha zao. Aidha, Waziri Mkuu amesema tayari ametoa maagizo kwa Wizara ya Kilimo na Bodi ya Mazao Mchanganyiko kuhakikisha mchakato wa uhakiki na kuwalipa wakulima wote unamalizika hadi kufikia Februari 15 mwaka huu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter