Home VIWANDAMIUNDOMBINU Mwendokasi kufika Mbagala

Mwendokasi kufika Mbagala

0 comment 111 views

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (Dart), Ronald Lwakatare amesema mradi wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka (Mwendokasi) kutoka Gerezani hadi Mbagala Kuu jijini Dar es salaam unatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa. Mtendaji huyo ameeleza kuwa ujenzi huo utafanyika pia kwenye barabara ya Kawawa kuanzia eneo la Magomeni, barabara ya Chang’ombe kuanzia eneo la Mgulani   hadi makutano ya barabara ya Kilwa na eneo la Mgujani JKT.

Pamoja na hayo, Lwakatare pia ameeleza kuwa, tayari wakandarasi wametia saini mkataba na Wakala wa Barabara (TANROADS) na kwamba mradi wa kwanza wa Sh. 189 bilioni utahusisha kilomita 20.3 za barabara huku mradi mwingine wa karakana moja, vituo vikuu pamoja na vituo vya barabara za kupishana magari ukigharimu Sh.48.82 bilioni.

“Ujenzi unaanza wakati wowote kuanzia sasa baada ya magari ya abiria kupisha katika vituo tulivyowaelekeza. Miradi hii miwili inasimamiwa na makandarasi wawili, wa majengo utakamilika kwa miaka miwili na wa barabara utakamilika kwa miaka mitatu. Watu wanaotakiwa kupisha mradi wameshalipwa fedha zao karibu wote, hivyo sasa wanatakiwa kupisha ili kazi ianze kufanyika haraka”. Amesema Lwakatare.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter