Home BIASHARAUWEKEZAJI Japan kufadhili miradi ya kijamii

Japan kufadhili miradi ya kijamii

0 comment 131 views

Japan imetoa ruzuku ya Dola za Marekani 277,445 nchini kwa ajili ya kutekeleza miradi mitatu Rukwa na  kisiwa cha Zanzibar. Kisiwani Zanzibar, fedha hizo zinategemewa kutekeleza mradi wa ujenzi wa bweni la wavulana katika shule ya sekondari Mohamed Juma Pindua iliyopo Pemba na mraji wa maji Unguja na kwa upande wa bara, fedha hizo zitatumika kununua mashine itakayotumika kwa ajili ya upasuaji mkoani Rukwa.

Balozi wa Japan nchini Shinichi Goto ameelezea kuwa ujenzi wa bweni kisiwani Pemba utagharimu Dola 130,179 za Marekani, mradi wa maji utatumia Dola 84,684 na mradi wa Benjamin Mkapa mkoani Rukwa utatumia takribani Dola 62,852.

Mradi wa Pemba upo chini ya Halmashauri ya Mji wa Pemba huku mradi wa maji ukiwa chini ya shirika binafsi linalohusika na mambo ya maendeleo na jinsi ya kukabiliana na umaskini. Mradi wa Rukwa unatekelezwa na taasisi ya Benjamin Mkapa.

Balozi huyo amefurahishwa na namna usimamizi wa miradi hiyo unavyoendelea hadi sasa na kusema serikali ya Japan itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuhakikisha miradi ya kijamii na kiuchumi inaendelezwa nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter